Brack Mustafa, msanii anayekua kwa kasi kutoka Malindi, Kaunti ya Kilifi, amevutia tena mashabiki wake kwa picha aliyoipakia kwenye mitandao ya kijamii. Mustafa, anayejulikana kwa uhusika wake wa kipekee katika tasnia ya burudani, alipakia picha hio akiwa na nguli wa Hip Hop tokea Mombasa Kaa La Moto na timu ya wasanii na watayarishaji wa muziki maarufu nchini.
Picha hiyo alipost na maandiko ya, “Stand for what you love and what you love will stand for you 🤍🙌🏼.” Ujumbe huu umeacha mashabiki wakihisi wasiwasi kuhusu hatua kubwa inayofuata ya Mustafa.
Kaa La Moto, ambaye alikuwa kwenye picha hiyo, aliandika maandiko yaliyosema: “Meeting of minds 🙏,” ambayo yameongeza hamu ya mashabiki kujua zaidi kuhusu ushirikiano huu.
Maelezo kuhusu mradi huu unaowezekana bado haijawekwa wazi, huku mashabiki wakiwa na hamu kubwa ya kujua kinachoandaliwa. Wakati ulingo wa burudani ukijiandaa kwa habari hizo, tutawajuza mashabiki kuhusu hatua zinazofuata za Brack Mustafa.