DJ Kezz. PHOTO/@DJKezzKenya/Instagram

Mchezaji Santuri wa Injili maarufu na mwanamuziki Keziah Jerono, anayejulikana kama DJ Kezz, hivi karibuni alifunguka kuhusu maisha yake katika mahojiano na YouTuber maarufu humu nchini.

DJ Kezz alizungumzia miaka yake ya changamoto, ambayo ilihusisha tukio la kuteswa na ujauzito wa ghafla, na kusababisha kufukuzwa kwake kutoka Kanisa la Seventh-Day Adventist (SDA).

Aliweka wazi kuwa akiwa na umri wa miaka 17, alipoenda kwa mara ya kwanza kwenye klabu huko Eldoret, alidanganywa kwa mbinu za hila na hivyo kupelekea yeye kupata ujauzito. Hakumweleza mtu yeyote kuhusu tukio hilo wakati huo.

“Nikiwa na umri wa miaka 17, nili***** na kupata ujauzito baada ya kwenda kwa mara ya kwanza kwenye klabu. Nilichagua kutosema kwa mtu yeyote,” alisema DJ Kezz. Baada ya ujauzito wake kugundulika, alikumbana na adhabu kali, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kutoka kanisani na kutengwa na jamii.

“Wakati watu walijua, naelewa kwamba kanisa lina taratibu kali, hasa katika maeneo ya vijijini. Kutengwa kulikuwa siyo kutoka kwa kanisa tu bali pia kutoka kwa marafiki na jamii,” alieleza.

Kutengwa kwa kanisa kulimfanya kuwa na hasira na kutokuelewana na Mungu, ingawa alijua kwamba siyo kosa la Mungu. Hali hiyo ilimpelekea kuacha kanisa mnamo mwaka wa 2017 na kuanza kazi ya kuwa DJ wa klabu.

“Kufukuzwa kwa kanisa kuliniacha nikiwa na hasira, lakini nilijua kwamba siyo kosa la Mungu. Nilihamasika kujiingiza kwenye DJaing,” alishiriki. Safari yake ya kucheza santuri ilianza alipokuwa chuoni, ambapo alihudhuria sherehe na kujiingiza katika sanaa hiyo.

“Wakati nikiwa chuoni, nilianza kwenda kwenye sherehe, na nikiwa kama mama mchanga, niliingia kwenye ulimwengu wa DJ. Hapo ndipo safari yangu ya DJ ilipoanzia. Kwa karibu miaka sita, sikuingia kanisani,” aliongeza DJ Kezz.

Mnamo mwaka wa 2020, DJ Kezz alianza safari ya kiroho ya kujirekebisha. Kipindi cha uviko19 kulimpa fursa ya kuunganishwa tena na imani yake na kutumia vipaji vyake vya DJ kueneza ujumbe wa Mungu kwa hadhira pana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *