Mashabiki wa Kilifi wamepata tuzo ya Mashabiki Bora katika mashindano ya Dola Super Cup baada ya kuonyesha msisimko na uaminifu wa kipekee wakati wa fainali za mwaka huu. Tuzo hii inatokana na mwitikio wa kupigiwa mfano waliouonyesha, wakiwa na shauku kubwa kuishangilia timu yao kuanzia sekunde ya kwanza hadi walipopata ubingwa pale Mombasa sports club.
Kama sehemu ya tuzo, mashabiki wa Kilifi wamejishindia shilingi elfu hamsini. Hii ni baada ya kuonekana wakishiriki kwa umoja na ari, wakiunga mkono timu yao kwa nguvu zote.
Wadhamini wakuu wa Dola Super Cup wametoa pongezi kwa mashabiki wa Kilifi, wakisema walipongeza nidhamu yao na mapenzi yao makubwa kwa timu yao. “Nidhamu na mapenzi ya dhati kutoka kwa mashabiki wa Kilifi yalikuwa ya kipekee. Walikuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha timu yao na kuifanya iweze kufika mbali,” walisema wadhamini.
Hii ni ishara ya wazi ya jinsi mashabiki wanavyoweza kuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya timu yao, na ushindi huu ni ushuhuda wa upendo na uungaji mkono ambao mashabiki wa Kilifi wameuonyesha kwa timu yao.