Beka Ruga an Actor and Comedian

Mtumizi maarufu wa mitandao Beka Ruga ”Batoto Ba Msambweni.” aliibua mzozo mkubwa baada ya kutoa ombi lililoshangaza wafuasi wake. Katika posti aliyoweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, Beka Ruga alieleza kuwa endapo Kilifi ingeshinda fainali za Dola Super Cup, angeomba watu wa Kilifi wamvue nguo na kumchapa viboko hadharani kutoka Mombasa Sports Club hadi Ferry, bila serikali kuingilia kati.

 “Mimi BEKA RUGA Nikiwa na Akili Zangu Timamu, Nasemaje Ikitokea KILIFI Wakishinda Finals Za DOLA SUPER CUP Jumapili Basi Watu Wa KILIFI WANIVUE NGUO WANICHAPE VIBOKO HADHARANI Kutoka MOMBASA SPORTS CLUB Hadi Ferry Na Serekali Isiingilie kati!” Beka alisema.

Aidha, Beka aliongeza kuwa hana imani kwamba Kilifi wana uwezo wa kushinda zawadi ya milioni moja ya dola, akisema: “Kilifi Hamna Uwezo Wa Kushinda 1 Million Ya Dola Hata Mkaroge Wapi. Mana Mpira Hamjui. KOMBE LINA BAKI MOMBASA MPENDE MSIPENDE.”

Matamshi haya ya Beka Ruga yameibua hisia mseto miongoni mwa wafuasi na mashabiki wa soka kwa sasa, huku wengine wakishangazwa na hatua yake ya kudharau uwezo wa Kilifi katika mashindano haya. Wengi wanajiuliza kama Beka atashikilia msimamo wake endapo Kilifi watatimiza malengo yao na kushinda taji hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *